Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkaribisha Mratibu Mkazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez alipomtembelea kwa
ajili ya mazungumzo.
Mratibu
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez,
alikutana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na kufanya
naye mazungumzo.
Miongoni mwa mambo waliyojadili ni maandalizi ya shughuli na matukio kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa (UN@70 ).
Katika
mazungumzo yao walikubaliana kufanya shughuli ya upandaji miti
kuzunguka Mlima Kilimanjaro na kusafisha sehemu ya mji kabla ya Siku ya
Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa mkoa alikubaliana na wazo hilo na kusema shughuli hiyo inafaa kufanyika katikati ya mwezi wa Agosti.
Wawili hao wakipiga picha ya pamoja.
Wakiagana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269