Breaking News

Your Ad Spot

Jul 29, 2015

CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAITAKA TUME KUONGEZA VIFAA PAMOJA NA RASILIMALI WATU ILI KURAHISISHA UANDIKISHAJI DAFTRAI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.


Chama Cha Mapinduzi  mkoa wa  Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi  alisema anawashukuru waandishi kwa ushirikiano waliounesha  kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa urais  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.
Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani na Ubunge .
Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na  shauku ya kutaka kujua maoni ya  CCM juu ya kuondoka kwa Edward  Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages