Breaking News

Your Ad Spot

Jul 9, 2015

MANCHESTER UNITED WANATAKA KUMNASA MKALI HUYU…KABLA HAWAJATUA MAREKANI KUANZA JARAMBA

Man UManchester United wameanza tena mazungumzo na klabu ya Southampton juu ya Morgan Schneidrling, Sportmail limeripoti kuwa muwakilishi wa Old Trafford alisafiri Jumatano kuelekea South Coast kwa ajili ya kuhakikisha dili la kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa linafanikiwa.United awali waliweka mezani ofa ya pauni milioni 20 kwa ajili ya kumnasa Schneiderlin lakini ilikataliwa na kocha wa Southampton Ronald Koeman.

Man U 1Mazungumzo kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo mwenye miaka 25 yalisitishwa, lakini yameanza tena na inawezekana Man United wakaongeza mzigo kwa ajili ya kuhakikisha wanaipata saini ya nyota huyo.
Kocha wa ‘Mashetani Wekundu’ Louis van Gaal anataka kumsajili Schneiderling kabla kikosi chake hakijaondoka kuelekea Marekani kwenye ziara ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao (pre-season tour).
Inaelezwa kuwa Southampton wanahitaji kitita cha pauni milioni 27 ili imuachie mkali huyo ambaye pia anazivutia klabu za Arsenal na Liverpool.
Man U 2Lakini kwa upande wa United wao wanaamini kuwa, kiungo huyo atakuwa ni mbadala wa Michael Carrick na wanapewa nafasi kubwa ya kuipata saini ya mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages