.

MANCHESTER UNITED YAITANDIKA BARCELONA BAO 3 -1

Jul 26, 2015

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Barca waliweza kuonesha kumiliki mpira kwani waliweza kupiga pass 314 kwa 198 huku zikiwa zenye asilimia 90.8 dhidi ya zile 80.8 za Manchester United.
Manchester United Usiku wa Kuamkia jumapili ya tarehe 26/7/2015 waliweza kuandika historia katika Mchezo wa soka kwa kucheza Mechi na Magwiji wa soka kutoka Hispania timu ya Barcelona na Hadi kupyenga cha Mwisho ni Machester United iliyoibuka kidedea kwa Ushindi mnono kabisa wa Mabao 3 - 1 dhidi ya Barcelona.
Ni Manchester United ambao walikuwa wakwanza kuandika bao la Kwanza mnamo dakika ya 8 ya mchezo huo kupitia kwa Mchezaji Wayne Rooney ambaye alifunga Goli hilo baada ya Mpira wa Kona kupigwa na Ashley Young na Kumkuta yeye na kupiga Kichwa safi kabisa na kumuacha Mlinda mlango wa Barcelona Ter Stegen akishindwa kuokoa Mchomo huo.
HADI MAPUMZIKA MATOKEO YALIKUA Manchester United 1 - Barcelona 0

Mnamo dakika ya 60 ya Kipindi cha pili Suarez aliweza kupachika bao na kuanza kushangilia lakini bao hilo liliweza kubatilishwa na Mshika kibendela ambae alionyesha kuwa alikuwa amekwisha Jenga kibanda kabla ya Kufunga bao hilo.
Wakati huo huo Kocha wa Manchester United aliweza kufanya Mabadiliko katika kikosi chake kwa kuwatoa wachezaji 11 na mabadiliko hayo yaliweza kuleta matunda kwani dakika nne baadae Lingard aliweza kuiandikia timu yake Bao la Pili katika mchezo huo.
Mnamo dakika ya 67 Adnan Januzaj angeweza kufunga goli la tatu lakini alipaisha mpira baada ya kupiga shuti lililokosa macho na kutoka nje.
Barcelona waliwezakufanya mabadiliko kwa Sandro Ramírez kuchukua nafasi ya Pedro, Gerard Gumbau kwa Andrés Iniesta, Alen Halilovic kwa Sergio Busquets, Marc Bartra kwa Gerard Piqué na Munir El Haddadi akichukua nafasi ya Luis Suárez.
Wakati huo kikosi cha United kilikuwa ni Johnstone, Valencia, Smalling, McNair, Blackett, Lingard, Fellaini, Herrera, Wilson, Pereira, Januzaj

Rafinha aliweza kuiandikia bao pekee kwa upande wa Barcelona mnamo dakika ya 89. Lakini goli hilo halikuweza kudumu kwani dakika moja baadae Adnan Januzaj aliweza kuifungia Manchester United Goli la 3 na la ushindi katika Mechi hiyo.

Huu utakuwa ni Ushindi wa Mechi tatu mfululilo kwa Manchester United.

VIKOSI: United XI: De Gea, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Mata, Young, Memphis, RooneyStarting XI: Ter Stegen, Piqué, Sergio, Pedro, Iniesta, Suárez, Rafinha, Alba, S.Roberto, Adriano, Vermaelen

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª