.

MAPOKEZI YA DK. MAGUFULI YATIGISHA DAR, WANANCHI KWA MAELFU WAFURIKA VIWANJA VYA ZAKHEM, MBAGALA KUMSHUHUDIA

Jul 14, 2015

 Wananchi kwa maelfu wakiwa wamefurka kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala, Dar es Salaam, wakati Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli (kushoto), alipowahutubia kwenye viwanja hivyo wakati wa mapokezi yake, leo.
 Mgombea mwenza wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli (kushoto), Samia Suluhu, akiwasalimia wananchi wakati, Dk. Magufuli namgombea mweza huyo walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo na kufanyiwa mapokezi makubwa
Dk. Magufuli akizungumza wakati wa mapokezi yake, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.
 Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
 Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli .
 Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.
 Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofika kumshuhudia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala Dar es Salaam, leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwahutubia maelfu ya wananchi, walioofika kumshuhudia mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala, Dar es Salaam, leo.
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, akiwasalimia maelfu ya wananchi waliofika kumshuhudia kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala, Dar es Salaam, leo
Mgombea Mwenza wa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli,  Samia Suluhu akiwa na mbnge wa Temeke, Abbas Mtemvu wakati wa mkutano wa mapokezi yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, akiwahutubia maelfu ya wananchi waliofika kumshuhudia kwenye Viwanja vya Zakhem, Mbagala, Dar es Salaam, leo
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa mapokezi ya Dk. Magufuli kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akisistiza jambo

Mgobea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakizicharaza tumba, kusaidia wakati bendi ya TOT Plus ilipokuwa ikitumbuiza wakati wa mapokezi ya mgombea huyo kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo
Umati wa maelfu ya wananchi waliofurika kwenye Viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam, leo kumshuhudia mbomgea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli leo. Picha zote na Adam Mzee

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª