Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi
wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu
wanaoeneza malaria kilichogharimu kiasi cha bilioni 61.5 za kitanzania,
ambapo alipongeza mradi huo kwani utasaidia kuondoa ugonjwa wa malaria
nchini, pia aliipongeza sekta ya afya kwa kusaidia kupunguza vifo
vinavyotokana na malaria kwa asilimia 71 na wagonjwa wenye kuugua
malaria kwa asilimia 51 kwa kipindi cha mwaka 2004-2014 leo Mjini
Kibaha.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria
Mh.Hailemariam Dessalegn akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda
cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria
ambapo aliipongeza serikali ya Tanzania katika kutekeleza Mradi huo
utakaosaidia katika kupambana na vita dhidi ya malaria nchini Tanzania
na Afrika kwa Ujumla, leo Mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha
kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo
alishukuru na kupongeza uzinduzi wa kiwanda hicho kwani kitakuwa ni
mwarobaini katika mapambano dhidi ya malaria kwa mkoa wa pwani na afrika
kwa ujumla,leo Mjini Kibaha.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.
Abdalah Kigoda akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha
kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria na
kuahidi kushirikiana kwa karibu na shirika la maendeleo ya taifa (NDC)
katika kutekeleza majukumu ya kiwanda hicho ili kutekeleza agizo la Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika vita dhidi ya malaria kupitia Mradi
huo, leo Mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa
Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya
Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda
cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria
leo mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant mzindakaya akimkabidhi zawadi Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa
hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi
vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria
Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete wakifungua jiwe la msingi wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu
wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria
Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha
kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo
mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria
Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria
Mh.Hailemariam Dessalegn akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wakati wa Halfa ya uzinduzi wa
kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza
malaria, leo mkoani Pwani, Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Balozi wa Cuba nchini Tanzania
Bw. Jorge Luis Lopez akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha
kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria
kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Cuba na Tanzania, ambapo
aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika masuala balimbali ya
maendeleo leo mkoani Pwani.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu
vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO
kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu
vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani
Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.(Picha na Freddy
Maro).
…………………………………………………………………..
VICTOR MASANGU, KIBAHA-PWANI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Kikwete amesemaSerikali ina mpango wa nchi nzima wa kupulizia dawa kwa ajili ya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria lengo ikiwa ni kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Dokta Kikwete ameyasema hayo
jana wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya kuua
viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria kilichopo eneo la TAMCO wilaya ya
Kibaha Mkoani Pwani.
Raisi Kikwete alisema Serikali
imekua ikipambana na ugonjwa huo kwa kutumia dawa za malaria za Mseto
na baadae Vyandarua vyenye dawa za kuua wadudu wa ugonjwaambavyo
vilisambazwa kwa nchi nzima huo lakini bado haijafanikiwa kuuondosha
kabisa hapa nchini pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika.
Alisema Kiwango cha maambukizi
ya ugonjwa huo kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia 10
mwaka 2012, ambapo pia idadi ya wagonjwa imepungua kutoka asilimia 51na
vifo vimepungua hadi asilimia 71 kutoka mwaka 2004 hadi 2014..
Aidha Dokta Kikwete aliwataka
wananchi kuendelea kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata
maambukizi ya ugonjwa huo na kuondokana na dhana potofu kuwa vyandarua
hivyo vinasababisha madhara hususani kwa wamnaume.
Kwa upandewake Waziri wa
Viwanda na Biashara Abdallah Kigoda alisema mikakati ya serikali ni
kuongeza viwanda mama kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza kasi ya
ugonjwa wa malaria ambao umekua kikwazo cha maendeleo kwa wananchi.
Waziri huo pia alibainisha kuwa Serikali ina mikakati ya kufufua bandari za nchi kavu na majini ikiwa sambamba na kuboresha miundombinu ya reli ili kuwezesha kufika kwa urahisi kwenye maeneo ambayo yalikua vikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kujenga viwanda na kuongeza fursa mpya ya ajira kwa watanzania hususani vijana ambao wataongeza pato la Taifa.

Waziri Mkuu wa Ethiophia na
mwenyekiti wa kupambana na malaria barani Afrika HaileMariam Desalegn
ataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha mapambano
dhidi ya ugonjwa huo inaendelea kwa nchi za Afrika.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya NDC
Christopher Mzindakaya alisema kuwa hadi sasa kiwanda hicho kimewaajiri
wafanyakazi 145 na kimegharimu kiasi cha shilingi bilion 61.5 hadi
kukamilika kwake pia kitakua na uwezo wa kuzalisha lita za ujazo milioni
sita kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269