Kaimu
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto),
akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es
Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na
Dharura, Dk.Elias Kwesi.
Mkurugenzi
Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia),
akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo.
Ofisa
Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry
Kessy (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada
kwenye semina hiyo.
Mkaguzi wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Mossi Ndozero (kulia), akitoa mada kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry
Bantu akizungumza kwenye semina hiyo.
Mkuu
wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Mary Kitambi akitoa mada kuhusu sekta ya Afya inavyokabiliana na
changamoto za utoaji huduma kwa wagonjwa wanaopata ajali.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikifunguliwa.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye
semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
Dotto Mwaibale
WATOTO
1, 86, 300 wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za magari
duniani hivyo kuwa changamoto kubwa ya usalama barabarani.
Hayo
yalibainishwa na Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya
Duniani (WHO), Marry Kessy wakati akitoa mada kwa wanahabari kwenye
semina ya siku moja ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani
iliyofanyika Dar es Salaam leo.
"Hii
ni changamoto kubwa duniani na hapa nchini kwani kati ya watoto hao
idadi kubwa ya wanaopoteza maisha katika ajali hizo ni watoto wa kiume"
alisema Kessy.
Mkaguzi
wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Mossi
Ndozero alisema kumekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na masuala ya
usalama barabarani ikiwemo ukiukwaji wa sheria za barabarani
unaosababishwa na binadamu.
Ndozero
aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani na
kufuata sheria jambo litakalo saidia kupunguza changamoto hiyo ya ajali
kama sio kuisha kabisa.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema maendeleo ya
dunia yamesababisha ongezeko la magari barabarani hususan nchini
Tanzania hivyo kuongeza ajali za barabarani.
Bantu
aliwataka watanzania kujenga utamaduni wa usalama barabara ambao hatuna
jambo litakalo saidia kupunguza ajali kwa kusaidiana na wadau wengine.
Mkuu
wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Mary Kitambi alisema ajali zinazotokea nchini zimechangia kuwepo kwa
ongezeko kubwa la wagonjwa hivyo kuwa changamoto katika hospitali
mbalimbali nchini kutokana na wodi kutokidhi ongezeko la wagonjwa na
vifaa tiba.
Alisema
kilele cha maadhimisho ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama
barabarani yatafanyika Julai 15 mwezi huu Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269