Mmoja
wa wafanyakazi wa benki ya Maendeleo ya Wakulima, Geofrey Mtawa
akizungumza na moja ya wadau waliotembelea banda lao katika maonyesho ya
Nanenane.
Na Mwandishi wetu
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania inashiriki maonesho ya kilimo ya
Nanenane kitaifa kwa mara ya kwanza mkoani Lindi mwaka huu kwa lengo la
kutambulisha huduma zake kwa wadau wake wakuu, wakulima.
Katika
maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi jana jumanne na Waziri Mkuu Mh.
Mizengo Kayanza Peter Pinda, benki hiyo inatoa elimu na kujitambulisha
kwa wakulima kwa kuwaelezea huduma zake zenye lengo la kuanzisha mtizamo
mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali,
kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na
ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati
na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo.
Akifungua
maonesho hayo Waziri Mkuu Mh. Pinda, alisema kuwa Nanenane ni shamba
darasa kwa wakulima kwa kuwa kupitia maonesho hayo wakulima watajifunza
mbinu mbalimbali zenye kuongeza tija katika kilimo chao, na pia
kujifunza wapi wanaweza kupata msaada kwa ajili ya kuinua kilimo chao
sambamba na kujua namna wanavyoweza kutumia zana za kisasa ili kuongeza
tija katika kilimo.
Benki
ya Maendeleo ya Wakulima imeanzishwa maalum kwa ajili ya kuinua kilimo
na itakuwa ikitoa huduma za uwezeshaji kwa wakulima na wafugaji kupitia
wadau mbalimbali wa katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha kuwa pamoja
na mambo mengine wakulima wa kitanzania wanafikiwa na zana za kilimo
kama vile mbegu za kisasa, pembejeo, uwezeshaji wa vifaa vya usindikaji
mazao ili kuongeza tija katika shughuli za kilimo.
Kwa
wadau wanaotembelea banda lake hapa Nanenane, warapata fursa ya kuona
vibanda vidogovidogo baadhi vikisheheni wakulima, wasindikaji na wauzaji
wa bidhaa walizochakata wenyewe kutoka mashambani kwa upande mmoja
lakini pia wako wadau wanaowezesha wakulima kama vile taasisi za utafiti
wa mbegu za kilimo, wauzaji wa zana za kilimo kama SUMA JKT ili
kuisaidia benki hiyo kufafanua namna itavyowezesha mfumo wa killimo na
kuhakikisha kuwa mkulima anapata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.
Benki
ya Maendeleo ya kilimo Tanzania inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe
nane katika kilele cha maonesho haya ya Nanenane na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Muonekano wa nje wa banda la benki ya wakulima la Nanenane.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269