Baadhi ya waandishi pamoja na viongozi wa Night Support wakiwa katika kikao
Mazoezi yakiwa yanaendelea
Baadhi ya watumishi
Baadhi ya Magari ya Night Support
KAMPUNI ya ulinzi ya Knight
Support yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam imefungua huduma mpya za
uokoaji wa maisha ya binadamu na zimamoto jijini Mbeya.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa huduma hizo uliofanyika juzi katika viwanja vya Hoteli ya Mbeya,
Meneja Mkuu msaidizi wa Knight Support, Ahmir Malik, alisema wamekuja Mbeya ili
kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za uokoaji kwa kuleta gari la
kubebea wagonjwa na gari la zimamoto.
Alisema lengo la kuleta huduma
hizo mkoani Mbeya ni kutokana na kupata mafanikio makubwa katika huduma ya
ulinzi ambayo ilipokewa na kuitikiwa kwa wingi ikiwa ni pamoja na kampuni
kujitanua kibiashara.
Naye Meneja mauzo wa Kampuni
hiyo, Farry Desouza, alisema huduma za uokoaji zitafanywa kwa mteja kuchangia
fedha kidogo ambazo zitaainishwa baadaye lakini pia kazi za kujitolea kama
zitatokea kama vile kikosi cha uokoaji cha Halmashauri ya Jiji kikishindwa
jambo kinaweza kuomba msaada Knight Support wakasaidia.
“Hatujaja kushindana naserikali
bali ni kushirikiana kwani kunaweza kukatokea tatizo kubwa ambalo Fire ya Jiji
ikashindwa kulimudu wakatuomba tukasaidiana vile vile hata sisi tunaweza
kuzidiwa hivyo inakuwa rahisi kuomba msaada kutoka serikalini” alifafanua
Meneja masoko.
Aliongeza kuwa watakuwepo
wateja wa kudumu ambao wataweza kulipia huduma kwa Mwaka au mwezi ambao
watafungiwa vifaa maalumu ambacho akibonyeza kulingana na tatizo atapata msaada
wa haraka lakini kwa wateja wengine kutakuwa na huduma za simu ya mkononi itakayopokelewa
masaa 24.
Kwa upande wake Meneja wa
Kampuni hiyo Mkoa wa Mbeya, Harrison Kilai, alisema huduma zitakazotolewa
zitakuwa na ubora mkubwa kutokana na vijana watakaofanya kazi hizo kupata
mafunzo ya kutosha na kufaulu kutoka kwa wakufunzi ambao ni raia wa Uingereza
waliobobea katika maswala ya uokoaji.
Alisema vijana 8 ambao ni
wakazi wa Mkoa wa Mbeya wamefuzu mafunzo ya huduma za afya ambao watatoa huduma
ya kwanza na kuendesha gari la wagonjwa vivyo hivyo vijana 11 wamefuzu mafunzo
ya zimamoto na uokoaji.
Aliongeza kuwa wamelazimika
kwenda sambamba na uokoaji na gari la wagonjwa kutokana na watu wengi kupata
madhara wakiwa kwenye majanga hivyo wakati zimamoto likiendelea kuokoa na
waliopata madhara watabebwa na kupewa msaada wa haraka kwenye gari maalum huku
akikimbizwa hospitalini.
Na Mbeya
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269