.

KATIBU WA BASEBALL TANZANIA AIKABIDHI TIMU YA TAIFA YA MCHEZO HUO JIJINI DAR ES SALAAM

Aug 19, 2015

2
Bw. Alferio Nchimbi Katibu wa Chama cha Mchezo wa Baseball na Softball Tanzania akikabidhi vifaa vya michezo kwa wachezaji wa timu ya mchezo huo ya Tanzania inayotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Uganda kwa ajili kambi ya mafunzo ya Meja League Base Ball Training Camp For Tryout (MLB) yatakayofanyika kuanzia tarehe 23-25 Agosti 2015 ambapo wachezaji watakaochaguliwa kutoka katika kambi hiyo watakwenda nchini Afrika Kusini kwa kwa mafunzo ya wiki mbili na baadaye wachezaji watakaochaguliwa kutoka kambi ya mafunzo ya Afrika Kusini watakwenda katika mafunzo kama hayo nchini Marekani kwa ajili ya kupata mafunzo zaidi ya mchezo huo na Scholarship ya kusoma nchini humo
Wachezaji waliochaguliwa katika timu hiyo ya taifa kwenda nchini Uganda ni Abdallah Abdallah kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir, Pius Cheka kutoka Sekondari ya Kibasila, Martin Cosmas kutoka Sekondari ya Azania, Juma Fikiri na Leodgar Leonidas kutoka sekondari ya Azania. Timu zitakazoshiriki katika mafunzo hayo ni Tanzania, Kenya na Uganda
Katika Picha kutoka kushoto ni Mwalimu Marck Hatia , Juma Fikiri, Martin Cosmas na Leodgar Leonidas wachezaji wa timu hiyo waliopokrea vifaa hivyo kwa niaba ya wenzao.
3

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช