Wasanii wa Kundi la The W.D kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% 2015 lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oystebay Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaunda kundi la Timu Makorokoro wa wilaya ya Temeke jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Vijana wanaaunda kundi la timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo iliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.(P.T)
Vijana
wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwalani jijini Dar es
Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la
robofainali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja
vya Donbosco Oysterbay jijini Da res Salaam ambapo makundi 10 yalitinga
nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni. Shindano hilo limeandaliwa
na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kundi la
wasichana pekee la Cute Babies kutoka Keko wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam wakionyesha umahiri wao wa kudansi wakati wa robo fainali ya
shindano la Dance 100% lililofanyika katika viwanja Don bosco Oysterbay
jijini ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi
karibuni, Shindano hilo liliandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom
Tanzania.
Baadhi
mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakifuatilia mchuano wa robo fainalai ya
shindano la Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV nakudhaminiwa na
Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa
kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
Makundi
kumi kati ya makundi 15 yaliyoshiriki katika kinyang’anyiro cha kuingia
katika nusu fainali ya mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya
Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV)
chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania,yanaendelea ambapo mwishoni mwa wiki tulishuhudia hatua ya robo
fainali kufanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es
Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es
Salaam.
Makundi
yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali ni Wazawa Crew,Majokeri,Quality
boys,The best,The best boys kaka zao,Team Makorokocho,The winners, The
W.D, Cute babies na Team ya shamba.Mratibu wa mashindano hayo,Happy
Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo walipata
makundi 10 hayo ambayo yameingia moja kwa moja katika ngazi ya nusu
fainali.
“Huu ni
mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya chini ya
udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya
yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila
kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki”Alisema Shame.
Shame,
aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya
ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East
Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha
shilingi milioni 5.
Naye
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa
mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa
kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa
vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema
kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira
hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo
makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa
mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la
ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Vodacom
tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta
mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya
tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na
kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia
katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Aliwataka
vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama
hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi
ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato
mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom
siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana
kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269