Breaking News

Your Ad Spot

Aug 17, 2015

MKUTANO WA MAJADILIANO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA YA JAPAN JUU YA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2015/16

nye1
Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (aliyesimama) akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto kwake ni Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango. Wengine ni Bibi Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa kwanza kulia), Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa tatu kulia).
Na: Thomas Nyindo
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
nye2
Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe huo MhandisiHappiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
nye3
Ujumbe kutoka Serikali ya Japan ambao unajumuisha Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan wakifuatilia mjadala kwa makini.
nye5
Wajumbe wakifuatilia majadiliano hayo kwa umakini yatari kwa kutoa michango yao juu ya mada iliyoko mezani.
nye4
Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania (wa pili kushoto) akisistiza jambo wakati wa mkutano huo. Wengine pamoja nae ni wajumbe kutoka Serikali ya Japan.
………………………………………………………………….
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pamoja na majukumu mengine, inajukumu pia la kuratibu miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa serikali ya Japan kila mwaka.  Maandalizi ya mwaka huu yameshakamilika na mkutano wa majadiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania na Serikali ya Japan ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hotel ya Hyatt Regeny, The Kilimanjaro, Dar es Salaam. Majadiliano hayo kwa upande wa Serikali ya Japan yaliongozwa na Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania, kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Malengo ya mkutano huo ni kujua hatua iliyofikiwa katika maombi ya ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka Serikali ya Japan kwa mwaka 2014/15, kuwasilisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili kwa mwaka 2015/16, kujadiliana changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuboresha ushirikiano baina ya Serikali hizi mbili. Pia Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, iliwasilisha mawazo ya awali ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II).
Wizara zilizoshiriki katika Mkutano huo ni pamoja na Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Wizara ya Fedha.
Wizara zingine ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Mendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, na Tume ya Mipango – Zanzibar.
Kwa upande wa Serikali ya Japani taasisi zilizohudhuria ni pamoja na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages