Breaking News

Your Ad Spot

Aug 3, 2015

MKUU WA USALAMA WA ZAMANI BURUNDI AUAWA

Jenerali Nshimirimana
Watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa mkuu wa usalama wa zamani wa Burundi na mshauri mkubwa wa Rais Pierre Nkurunziza.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema Jeneral Adolphe Nshimirimana alikufa pale gari lake liliposhambuliwa katika mji mkuu, Bujumbura.
Umoja wa Ulaya umesema mauaji yake yamezidisha wasiwasi, na kwamba juhudi za upatanishi lazima zianze tena.
Burundi imepita katika miezi kadha ya ghasia baada ya Rais Nkurunziza kuania na kushinda muhula wa tatu wa uongozi.
Inafikiriwa kuwa Jenerali Nshimirimana bado alikuwa na mchango mkubwa katika usalama, hata baada ya kutolewa kuwa mkuu wa usalama nchini Burundi.
Muandishi wa habari wa Ufaransa ambaye alipiga picha za pahala jenerali huyo aliposhambuliwa, alikamatwa na kupigwa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages