Muasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mzee Peter Kisumo (pichani) amefariki dunia.
Mwanasiasa
huyo mkongwe nchini ambaye aliwahi kushika nyadhifa kadhaa katika
Serikali ya Awamu ya Kwanza, alifariki Dunia jana saa moja usiku katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wa
marehemu, Michael Kisumo alilithibitishia gazeti hili jana juu ya kifo
cha baba yake akisema kilitokana na maradhi ya figo ambayo yamekuwa
yakimsumbua kwa muda mrefu.
“Tulikuja
hapa Muhimbili kwa ajili ya mzee kufanyiwa dialysis (usafishaji damu
katika figo) sasa ikajitokeza complication (utata) akaanza kuharisha
damu,” alisema.(P.T)
Michael alisema baba yake alilazwa wodi ya kawaida juzi ili jana apatiwe tiba hiyo kabla ya hali yake kubadilika ghafla.
“Daktari
wake alipokuja leo (jana) na kumwangalia aliagiza atolewe wodi ya
kawaida ahamishiwe ICU lakini ilipofika saa moja usiku akatutoka”
alisema Michael.
Kifo cha
mwanasiasa huyo kimekuja takribani mwezi mmoja tangu arejee kutoka India
ambako amekuwa akienda mara kwa mara kuchunguzwa afya yake.
Hali ya
ugonjwa wake huo ilifikia katika kiwango cha juu na kulazimika kufanyiwa
uchujaji wa figo mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.
Kisumo
aliwahi kuwa mmoja wa mameneja wa kampeni wa Rais Jakaya Kikwete mwaka
2005 akisimamia kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha na Tanga.
Mbali ya kuwa waziri, aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa na mdhamini wa CCM
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269