Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya
kurejea kutoka Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa
Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 akitokea Australia alikozuru
kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Peter Cosgrove.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 akitokea Australia alikozuru kwa
mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Peter Cosgrove.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar
es salaam, Ramadhani Madabida alipowasili katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi
Agosti 1, 2015 akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa
Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter
Cosgrove.
PICHA NA IKULU
---
Akiwa
nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri
Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua
kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba nchini
Tanzania.
Rais
Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Gavana
Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na
wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania
ambapo walizungumzia namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na
jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika kutokana na kupata gesi.
Tayari
Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta,
yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na tafiti
mbalimbali katika Kilimo.
Rais
Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa
heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake
mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa
madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269