.

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AZINDUA BARABARA YA KASKAZINI PEMBA

Aug 27, 2015

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba  katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi,
[Picha na Ikulu.]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifungua pazia kama ishara ya  kuifungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi.
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Juma Malik Akili (wa pili kushoto) na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakitembea katika  Barabara ya Wete-Gando baada ya kuizinduliwa rasmi juzi,katika katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba,
7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na wananchi wa katika Kijiji cha Ukunjwi katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba,akiwa katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo
4
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(kushoto) Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana, Wanawake na Watoto Bi.Zainab Omar Mohamed na Waziri wa Ardhi ,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakiwa sherehe za Uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde katika viwanja vya kijiji cha Ukunjwi Mkoa wa Kaskazini Pemba juzi,katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba
5
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Ukunjwi na Viongozi wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde zilizofanyika kijijini hapo Barabara iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein juzi katika ziara ya kuzindua miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Pemba,
6
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Mindombinu na Mawasiliano wakiwa katika sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Wete-Gando,Wete-Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,sherehe zilizofanyika viwanja kijiji cha Ukunjwi,

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช