Breaking News

Your Ad Spot

Aug 14, 2015

UJERUMANI YAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA SH. BILIONI 39.1 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA, MAJI NA MALIASILI.

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kulia) akisaini hati ya makubaliano katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar Es Salaam. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) katika hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, ujumbe wa ulioandamana na Balozi wa Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili 
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Egon Kochanke akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari mara baada ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili 
Viongozi kutoka Wizara ya Fedha, wajumbe kutoka Ujerumani pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 2 ya sekta za maji, afya na maliasili  Alhamisi Agosti 13, 2015 Jijini Dar Es Salaam

Na Jenikisa Ndile-MAELEZO 
Serikali ya Tanzania na Ujerumani zimetiliana saini mikataba miwili ya misaada yenye thamani ya jumla ya Euro milioni 17 ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni 39.1 kusaidia sekta ya afya, maji na maliasili.

 Makubaliano hayo yamesainiwa jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke ili kuleta mafanikio na maendeleo katika. 

 Aidha, Dkt. Likwelile amemhakikishia Balozi Kochanke na ujumbe wake kuwa msaada walioipa Serikali utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi na kuongeza nafasi za ajira na hatimaye kuchangia katika kuboresha uchumi nchini. 

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke amesema kuwa serikali ya Ujerumani itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuzingatia uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili. 

Zaidi ya hayo, serikali hizo mbili zimesaini mkataba wenye thamani ya Euro milioni 10 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 23 kuisaidia usimamizi wa hifadhi ya Taifa ya ya wanyama mwitu ya Selous

Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages