.

ZAIDI YA WAHAMIAJI HAMSINI WAMEFARIKI KATIKA PWANI YA LIBYA

Aug 28, 2015

Meli ya sweden ikishiriki katika operesheni ya uokoaji ya wahamiaji katika pwani ya Libya,Agosti 26, 2015.
Meli ya sweden ikishiriki katika operesheni ya uokoaji ya wahamiaji katika pwani ya Libya,Agosti 26, 2015.
Na RFI
Watu zaidi ya hamsini wamekutwa wamekufa katika sehemu ya mizigo ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji waliokamatwa katika pwani ya Libya, wakati wa operesheni ya kuwaokoa iliopelekea kuwapokea watu wengine 430 , mamlaka ya ulinzi katika pwani ya Italia imesema.
Meli ya Sweden (Poseidon), inayoshirikiana na ujumbe wa Ulaya Frontex ilitoa msaada kwa kuwaokoa wahamiaji hao ambapo miili kadhaa imegunduliwa.(P.T)
Ishara ya dhiki ilipokelewa hadi Jumatano wiki hii kwamba kuna boti kumi ambazo zinakabiliwa na matatizo, kwenye umbali wa zaidi ya kilomita hamsini na pwani ya Libya, msemaji wa mamlaka ya ulinzi katika pwani ya Italia.
Vyombo vya habari vya Italia vimebaini kwamba vifo hivyo vinaweza kuwa vimesababishwa na kukosa hewa.
Maelfu ya wahamiaji wamekufa na maelfu wengine kuokolewa baada ya kurundikwa katika meli moja hivi karibuni nchini Libya.
Mapema mwezi Agosti, Kikosi cha wanamaji cha Italia kiligundua miili ya watu arobaini na tisa katika meli moja.
Wahanga wa tukio hilo wamesema kuwa walilazimishwa kubaki katika chombo hicho ambacho kilijaa kupita kiasi.
Wasafirishaji haramu waliopo nchini Libya, wanaaminika kutengeneza faida kubwa kwa kuwasafirisha wahamiaji mpaka mwambao wa Ulaya.
Maafisa wa Ulaya wameelezea hatma ya wahamiaji, karibu 250,000 ambao wamesaifiri kwa boti mpaka ulaya.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa kwa mwaka huu pekee, zaidi ya wahamiaji 2,000 wamefariki dunia walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari na kwenda ulaya.
Wakati huo huo suala la uhamiaji linatarajiwa kutawala mkutano wa kilele mjini Vienna na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Ujerumani, Austria na nchi za Balkan.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช