Happy Limwamwa (9-10) Pichani
Happy Limwamwa 9-10 (kushoto) akizungumza kwa uchungu kwa Msaidizi wa
Kisheria Geophrey Kaduma, (wapili kulia) manyanyaso aliyokuwa akiyapata
toka kwa mama aliyekuwa amemtowa kwao Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma,
kwa malengo ya kufanya kazi za ndani, ndipo alipokutana na kichapo toka
kwa mama huyo na mume wake na kumfanya akimbiye na kuishi mitaani na
kuokotwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Bryceson Mgaya wa Mtaa wa Kambarage Kata ya Njombe Mjini Wilaya ya
Njombe Mkoa wa Njombe, Pamoja na Mwenyekiti huyo kutowa taarifa katika kituo cha Polisi na kumtembeza katika mitaa tofauti alipokuwa akifanya kazi zaidi ya wiki 3 bado juhudi yoyote haijazaa matunda kwa mtoto huyo kurudishwa kwao, kwa yoyote anaye weza kumfaham mtoto huyo awasiliane na Mwenyekiti huyo wa Mtaa, 0766336403, Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria Geophrey Kaduma, 0759601915-o655601915. wapili kushoto ni Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla na wakwanza kulia ni mke wa mwenyekiti wa Mtaa wa Kambarage Matha Maiseli (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Katibu wa Kituo cha Msaidizi wa Kisheria Magy Mtalla, akizungumza na mtoto huyo Happy Limwamwa 9-10
Happy Limwamwa 9-10 akiwa katika picha
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269