Breaking News

Your Ad Spot

Sep 29, 2015

BREAKING NEWS: NYOSSO AFUNGIWA KUCHEZA MPIRA KWA MIAKA MIWILI

Juma Said Nyosso, beki na nahodha wa kikosi cha Mbeya City anaetuhumiwa kumfanyia kitendo cha udhalilishaji mchezaji wa Azam FC John BoccoKamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages