Breaking News

Your Ad Spot

Sep 30, 2015

DAESH YAZUIA MIKUSANYIKO YA ZAIDI YA WATU WATATU

Daesh
Kundi la Daesh limepiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu watatu mjini Mosul huko Iraq, kutokana na kuongezeka upinzani wa wananchi wa mji huo dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Msemaji wa Chama cha Kurdistan Democratic Party KDP mjini Mosul, Saeed Mamouzini amenukuliwa akisema kuwa, kundi la Daesh limepiga marufuku mikusanyiko yote hata ya sherehe mjini Mosul.
Amesema, kundi hilo lina wasiwasi kwamba wananchi wa Mosul watamiminika mitaani kupinga udhibiti wa kundi hilo katika mji huo. Mosul ilitekwa na genge la Daesh tangu mwezi Juni mwaka jana.
Tarehe 31 Agosti mwaka huu, Mamouzini aliiambia televisheni ya al Sumaria kwamba kundi la Daesh limeua wanachama wake 112 huko Mosul ikiwatuhumu kupanga njama za kumuasi kiongozi wa genge hilo Ibrahim al Samarrai, maarufu kwa jina la Abu Bakr al Baghdadi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages