Breaking News

Your Ad Spot

Sep 27, 2015

DK MAGUFULI ATOA MPYA TENA AFANYA MAZOEZI YA NGUVU JUKWAANI MAKAMBAKO


 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akifanya mazoezi jukwaani akijiandaa kujinadi kwa wananchi katika Mji wa  Makambako, mkoani Njombe leo,  jambo ambalo lilizua vifijo, nderemo na vigelegele kutoka kwa wananchi waliofurika kwenye mkutano huo wa kampeni.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG





 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi kwa wananchi  kwa kuwaomba ifikapo Oktoba 25, mwaka huu wakati wa Uchaguzi Mkuu, waende wote kumpigia kura za ndiyo ili ashinde kwa kishindo urais.

 Wakazi wa Mwanjelwa, jijini Mbeya, wakimsikiliza Dk Magufuli akijinadi kwao baada ya msafara wake kuzuiwa eneo hilo ukitokea Uwanja wa Ndege wa Songwe ukienda Mbarali kuendelea na kampeni.

 Dk Magufuli akiomba kupigiwa kura na wananchi wa Nswisi wilayani Mbarali huku akirekodiwa na Shaban Kwaka wa TBC.


 Mama mkazi wa Igurusi wilayani Mbarali Mbeya, akifurahi baada ya kumuona Dk Magufuli.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Dk Magufuli akizungumza na wananchi wa Igurusi waliouzuia msafara wake



 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli alipokuwa akihutubia na kuomba kura kwao katika Mji wa Chimala, Mbarali mkoani Mbeya leo.

 Mfuasi wa CCM, akishangilia huku akiwa na picha ya Dk Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni Rujewa wilayani Mbarali, Mbeya leo.

 Waziri Mkuu mstaafu,  Samuel Malecela akitangaza wasifu wa Dk Magufuli na kwamba niye anayefaa kuchaguliwa kuwa rais tofauti na mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa.

 Sehemu ya wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni Rujewa leo

 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli wakati wa mkutano huo na kukubali kumpigia kura za ndiyo

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mbarali,

 Ni furaha iliyoje kwa wananchi wa Mbarali baada ya kufurahishwa na ahadi mbalimbali za maendeleo alizokuwa akizitoa kwaoPICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Dk Magufuli akimpokea mmoja wa wanachama wa chama cha ACT -Wazalendo aliyeamua kujiunga na CCM wilayani Mbarali

 Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge jimbo la Wanging'ombe, Gerson Lwenge katika Mji wa Ilembula, mkoani Njombe. Lwenge alikuwa Naibu waziri wa ujenzi wilazara iliyokuwa akiiongoza yeye

 Wananchi wa Ilembula wakimsikiliza Dk Magufuli akijinadi

 Moja ya mabango yalyokuwepo katika mkutano wa kampeni za CCM, mjini Makambako,

 Mgombea ubunge Jimbo la Makambako, Jah People akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Makambako ambapo pia alimuombea kura Dk Magufuli

 Huree Dk Magufuli

 Jah People akiibusu picha ya Dk Magufuli ikiwa ni ishara ya kumkubali kuwa rais

 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akitangaza wasifu wa Dk Magufuli na kwamba anafaa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuwa Rais wa Tanzania mjini Makambako, mkoani Njombe.

 Wananchi wakifurahia hotuba ya Dk Magufuli

 Dk Magufuli akiwa na baadhi ya waliovihama vyao vya upinzani na kuamua kujiunga na CCM wakati wa mkutano mjini Makambako



Dk Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mafinga, wilayani Mufindi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages