Kipa wa Nigeria Vincent Enyema,
amejiondoa kutoka kwa kikosi cha Nigeria, kitakachoshiriki katika mechi
ya kufuzu kwa fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka wa 2017,
dhidi ya Tanzania siku ya Jumamosi kufuatia kifo cha mamake.
Kocha
wa Nigeria, Sunday Oliseh, amesema kwa sasa Enyema, amepata pigo kubwa
na tumemruhusu kwenda nyumbani kwa misingi ya kibinadam.
Enyema alitarajiwa kusafiri Abuja siku ya Jumatatu, lakini alifutilia mbali safari hiyo.
Kipa
wa timu ya Uingereza ya Wolves, Carl Ikeme, anatarajiwa kujaza pengo
hilo katika mechi itakayokuwa ya kwanza katika timu hiyo ya Super
Eagles.
Enyema, anayeichezea klabu ya Ufaransa ya Lille na
mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha Super Eagles,
alikuwa kipa wa timu hiyo wakati ilipoicharaza Chad kwa magoli mawili
kwa moja mjini Kaduna mwezi Juni mwaka huu
Enyema ameichezea Nigeria mechi 101.
Misri ambayo haikushiriki
katika fainali tatu zilizopita, iliishinda Tanzania 3-0 mjini Alexandria
na sasa inaongoza kundi G, kutokana na wingi wa magoli.
Licha ya
kuwa timu zinazoogopewa zaidi barani Afrika, Nigeria na Misri ambao ni
mabingwa mara saba wa kombe hilo hawakufuzu kwa fainali iliyoandaliwa
nchini Equatorial Guinea mapema mwaka huu.
Wakati huo huo,
Shirikisho la mchezo wa Soka nchini Nigeria, NFF, limethibitisha kuwa
Super Eagles itakwaruzana na Mena ya Jamuhuri Ya Niger, katika mechi ya
kimataifa ya kirafiki tarehe 8 Septemba mjini Port Harcourt.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269