Breaking News

Your Ad Spot

Sep 20, 2015

KAMPENI ZA DK MAGUFULI KWAO CHATO NI ZAIDI YA TSUNAMI




Mgombea urais wa Tbanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato, mkoani Geita, jimbo alilokuwa Mbunge. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga wapiga kura wake.Mkutano huo wa kampeni ulijaza watu kupita kiasi  jambo ambalo wenyeji wa wilaya hiyo pamoja na mgombea amesema haijawahi kutokea.PICHA ZOTE NA RICHARD BMWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Mbuzi huyu aliyechorwa maandishi hayo aliletwa kwenye mkutano huo na mmoja wa wafuasi wa CCM kwa lengo la kuwakebehi Ukawa.

Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi wa Wilaya ya Chato ili wampigie kura nyingi yeye pamoja na mbunge na diwani wa CCM.

Dk Magufuli akiwahidi wananchi kuwa akipewa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha  elimu ya bure inatolewa kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne
Mke wa  Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Janeth Magufuli akipongezwa na mumewe, Dk Magufuli baada ya kutoka kumuombea kura 


Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza wakati wa mkutano huo



Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti



Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa juu ya magari kwa lengo la kupata picha nzuri wakati msafara wa Dk Magufuli ulipokuwa ukitokea nyumbani kwao kwenda kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato leo



Dk Magufuli akiingia kwenye mkutano wa kampeni mjini Chato

Kikundi cha ngoma za asili cha Mchele Mchele kikitumbuiza katika mkutano huo

Wanamuziki wa Yamoto Band wakitumbuiza  wakati wa mkutano huo



Wafuasi wa CCM wakionesha dole gumba ikiwa ni ishara ya kumkubali Dk Magufuli kuwa rais

Msanii Khadija Kopa wa Kikundi cha Sanaa cha CCM cha TOT, AKITUMBUIZA KWA WIMBO WA TAARABU WAKATI WA KAMPENI HIZO

Wasanii wengine wakiendelea kuunga mkono Malkia wa Mipasho Khadija Kopa



Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Abdallah Bulembo akielezea wasifu wa Dk. Magufuli uliomfanya ateuliwe na CCM kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Tanzania.

Dk Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Josph Musukuma wakati wa kampeni hizo

Mwakilishi wa watu wenye ulemavu wana CCM na wasio wanaCCM, Amon Mpanju akihutubia kwa kuelezea ubaya wa Ukawa na kusifia CCM ambayo alidai inawajali walemavu nchini.

Dk Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi wakiangalia vikundi vya sanaa vilivyokuwa vikitumbuiza katika mkutano huo

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Jpseph Musukuma akimwagia sifa lukuki Dk. Magufuli kuwa anafaa kuwa urais na kumponda mgombea urais  kupitia Ukawa ambaye alisema hafai kwani afya yake

Mke wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Janeth Magufuli akipita jukwaani baada ya kutoka kuhutubia na kuwaomba wananchi kumpigia kura mumewe ili ashinde urais wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Michezo mjini Chato.



Dk Magufuli akijipigia kampeni nyumbani kwao Chato

Dk Magufuli akiwaaga wananchi baada ya mkutano wa kampeni kumalizika  mjinbi Chato





Msafara wa Dk Magufuli ukipita kwenye taa za kuongozea magari ambazo alifanikisha kuziweka alipokuwa mbunge wa Jimbo la Chato







No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages