Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt
John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara
waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni
unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa.
Dkt John
Magufuli amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu
mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na
saruji,amesema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya
watanzania wote na hivyo atapunguza bei ya saruji na bati na hilo
litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo.
"Serikali
ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya
mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na
saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo
lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.
Alisema
anatambua kiu ya watanzania ni kutaka mabadiliko ya maendeleo na kwamba
Serikali yake itasimamia kuleta maendeleo ya wananchi na kazi hiyo
anaiweza na ndio maana anaomba urais. " Ndugu zangu watanzania serikali
ya Magufuli inakuja kuendelea pale ambapo awamu nyingine
zimeishia.Tumetoka mbali ,tupo mbali na tunakwenda mbali.Nataka tuwe na
maendeleo makubwa na hilo serikali yangu ndio kazi itakayofanya,"alisema
Dk.Magufuli huku wananchu wakimshangilia kwa mayowe.
Dk
Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya
Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo akishinda
uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile Eimu ya bure kutoka darasa
la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba
Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50
kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na
biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Dkt
John Pombe Magufuli,akiwahutubia wananchi wa mji wa Mtwara
waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye mkutano wa kampeni
unaoendelea jioni hii katika uwanja wa Mashujaa.
Dk
Magufuli tayari hadi sasa amefanya mikutano ya kampeni katika mikoa 6 ya
Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Mtwara. ambapo aakishinda
uchaguzi ameahidi mambo mbalimbali kama vile ile ya bure kutoka darasa
la kwanza hadi kidato cha nne, kujenga reli kutoka Mtwara hadi Mbamba
Bay mkoani Ruvuma, kushusha bei ya vifaa vya ujenzi na kutoa sh. mil. 50
kwa kila kijiji za kuwakopesha wanawake na vijana kuendeleza miradi na
biashara zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo
Wakazi wa
mji wa Mtwara wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara
wa kampeni za CCM,unaofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa
CCM,wakimsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.
Dk
Magufuli akizungumza na mtoto Riziki Faraji na pia alimpa kiasi kadhaa
cha fedha kwa ajili ya kununulia sare ya shule alipomuona wakati msafara
wake ulipozuiwa na wananchi katika Kijiji cha Kitama A, mkoani Mtwara
Dk
Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia
katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kata ya Ziwani Mtwara
Vijijini
Mgombea
Ubunge wa jimbo la Mtwara mjini,Murji Hasnein Mohamed akiwasalimia
maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara waliofurika kwenye uwanja wa
Mashujaa katika mkutano wa kampeni za CCM,jioni ya leo ambapo Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli aliwahutubia wananchi hao .
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akijiachia jukwaani pamoja na
wasanii wa kundi la Yamoto Band kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani
Mtwara,ambapo Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao waliofurika kwa
wingi.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269