Mwigulu
Nchemba na Mwakalebela wakiwa kwenye Gari ya wazi wakielekea Uwanja wa
Mwembetogwa hapa Iringa Mjini tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge.
Mwigulu
Nchemba akiingia na Gari la wazi kwenye Viwanja vya Mwembetogwa Iringa
Mjini kwaajili ya Kumnadi Mwakalebela anayepeperusha Bendera ya Chama
Cha Mapinduzi kwenye nafasi ya Ubunge.
Mwigulu
Nchemba ambaye yumo kwenye kikosi cha Timu ya Ushindi ya CCM, akiwasili
Viwanja vya Mwembetogwa kwaajili ya kuzindua Rasmi kampeni za Ubunge
Jimbo la Iringa Mjini kwa upande wa CCM
Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Iringa Mjini wakifuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za CCM Ubunge Jimbo la Iringa Mjini .
Ombi la Mdahalo kati ya Wagombea Urais halikupitwa kwenye mkutano huu wa kihistoria kwa Wananchi wa Iringa.
Mwigulu
Nchemba akizungumza na Maelfu ya Wananchi wa Iringa hii leo katika
Viwanja vya Mwembetogwa wakati akifungua Kampeni za Ubunge Jimbo la
Iringa Mjini ambapo CCM imemsimamisha Mwakalebela.
Wananchi wakiwatayari kusikiliza sera za chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Iringa kuelekea miaka 5 ijayoya Ubunge.
Mwigulu
Nchemba akiwasisitiza Wananchi wa Iringa kuwa ,Taifa letu linahitaji
Kiongozi Magufuli kwasababu anasifa ya Uchapakazi,Mwadilifu,Mtanzania
halisi,Sio mbaguzi na hana Urafiki kwenye kazi.Hivyo watanzania wampigie
Kura magufuli ifikapo October 25 Mwaka huu.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Iringa Ndg.Mwakalebela
Ndg.Mahiga
ambaye ni meneja kampeni wa Mwakalebela akiwatoa hofu wananchi wa
Iringa kuwa watafanya Kampeni za Amani na Utulivu na amewahakikishia
wataibuka washindi mapema October 25.2015.
Mwakalebela
ambaye ni Mgombea Ubunge akizugumza na Wananchi wa Iringa Mjini.Kubwa
amesisitiza kuwa anazijua kero za Wananchi wa Iringa Mjini hususani
maji,Miundombinu na huduma za Afya,Hivyo yupotayari kuwatumikia kwa
miaka 5 ijayo kama Mbunge wao.
Wananchi wa Iringa wakishangilia mara baada ya Mwigulu Nchemba kumsimamisha Mbunge Mtarajiwa Ndg.Mwakalebela.
Hisia za Wananchi kwa chama chao,Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu
Nchemba (katikati),Mbunge mtarajiwa Mwakalebela(kushoto) na Kampeni
Meneja wa Mwakalebela Ndg.Mahiga(Kulia) wakiwaaga wananchi wa Iringa
mjini na kuwashukuru kwa Mafuriko waliyoyaleta Uwanja wa Mwembetogwa.
Picha na Sanga Festo Jr.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269