Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
Waombolezaji
wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Anyosisye Mwakyusa, baba mzazi wa
mwandishi mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile, wakati
wa ibada ya kumuombea iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Ubungo Kibangu Dar es Salaam jana, kabla ya kuusafirisha
kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika leo.
Ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kuuga mwili wa mzee wetu Anyosisye Mwakyusa.
Familia ya marehemu ikiwa na huzuni wakati wa ibada hiyo.
Waomblezaji wakiwa ibadani.
Wafiwa wakipewa pole.
Mwanahabari Peter Ambilikile aliyefiwa na baba yake
akiwa katika huzuni.
Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo
Kibangu, Kishe Mhando (katikati), akiomba kabla ya kuanza kwa safari ya
kwenda mkoani Mbeya.
Mwili ukiondolewa kanisani.
Waombolezaji wakisubiri gari lililobeba mwili huo kuondoka kwendaa mkoani Mbeya kwa mazishi.
Ni huzuni tupu.
Na Dotto Mwaibale
MZEE
Anyosisye Mwakyusa ambaye ni baba wa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la
Jambo Leo, Peter Ambilikile mwili wake umeagwa jana kwenda mkoani Mbeya
kwa maziko.
Anyosisye alifariki juzi jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Ibada
ya kuaga mwili wa marehemu huyo ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu jijini Dar es
Salaam jana ikiongozwa na Mchungaji Kishe Mhando wa ushirika huo.
Mchungaji
Mhando alimwelezea Mwakyusa kama mtu jasiri ambaye siku zote alikuwa
mtu wa ibada na alikuwa akihudhuria ibada zote. Aliwaambia waumini kuwa
mshahara wa dhambi ni mauti na mshahara wa kuwa na ibada ni maisha ya
milele na Bwana Mungu.
Alisema
watu huwa wana ratiba yao na hakuna mtu hata mmoja anayejua ratiba ya
Mungu. "Msiba hauchagui mtoto mchanga, mtu mzima, mwanamke au mwanaume.
Mipango yote ni ya Mwenyezi Mungu, yeye ndiye anajua anayefuata ni
nani," alisema.
Mazishi
ya Mzee Mwakyusa yanatarajiwa kutafanyika mkoani nyumbani kwa marehemu
eneo la Makungulu jijini Mbeya leo. Mwakyusa alizaliwa Mei 10, 1942.
Alifunga ndoa yake mwaka 1968. Alifanya kazi serikalini na alistaafu
mwaka 1980.
Mwaka
1999 Mwakyusa alianza kulalamika kuwa na matatizo ya koo na kuanza
kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya
Ocean Road hadi kifo chake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269