Wachezaji
watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi,
Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana
Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars
iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.Kocha
Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana
kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa
10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.Kwa
mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na
mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi
mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
Wachezaji
waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma
Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani,
Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo
ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela,
Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa
na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho
Ngasa na Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269