,
MASHEIKH
sita wa Tanzania waliochukuliwa mateka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) wameachiwa huru usiku wa kuamkia jana.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Uhusiano wa Kimataifa, Liberata Mulamula, alisema Balozi wa Tanzania
nchini DRC kwa sasa yupo njiani kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,
Goma kwa ajili ya kuwaona mateka hao.
Alisema
taarifa za kutekwa watu hao zilitolewa mwanzoni mwa Agosti mwaka huu
ambapo Serikali ilifanya juhudi ya kufuatilia na kufanya uchunguzi juu
ya taarifa hizo.
Mulamula
alisema inasemekena watu hao wa taasisi ya kuhubiri dini ya Kiislamu
walitekwa na kikundi cha waasi ambapo hadi sasa hakijajulikana.
Alisema
watekaji wao walidai wapewe kiasi cha dola za Marekani 40,000 (sawa na
Sh milioni 128.7 ) ili wawaachie Watanzania hao huru ambapo waliwaomba
kupunguziwa hadi kufikia dola 20,000.
“Nchi
yetu haijawahi kutokea kukamatwa mateka, lakini tunaipongeza Serikali ya
DRC kulifuatilia hili na kutupatia taarifa,” alisema Mulamula.
Aliwataka
wananchi wanaokwenda nchi za ugenini kutoa taarifa katika ubalozi au
Wizara ya Mambo ya Ndani ili waweze kutambua haraka linapotokea tatizo
kama hilo.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya nje Zanzibar, Silima Kombo
Haji, alisema watekaji hao walitumia ujanja wa kupiga simu kwa ndugu zao
pamoja na watu wa karibu na Kijiji cha Goma.
Alisema
juzi watekaji hao walikuwa wakipiga simu wakisisitiza kuwa muda
umekwisha, hivyo fedha hizo zipelekwe haraka kabla hawajawadhuru.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269