Breaking News

Your Ad Spot

Oct 14, 2015

DK MAGUFULI ASHIRIKI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU DK KIGODA DAR

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akizungumza na vyombo vya habari jinsi alivyomfahamu aliyekuwa waziri wa Viwanda na Biashara, marehemu Dk Abdallah Kigoda wakati wa mapokezi ya mwili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dcar es Salaam jioni hii, ukitokea India ambako alipatwa na mauti.
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Mgombea ubunge Jimbo la Handeni kupitia CCM, marahemu Dk Abdallah Kigoda, ukihamishiwa kwenye gari lingine wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ukitokea nchini India ambako alipatwa na mauti. Mwili huo ulikwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, kusubiri kuagwa katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam

 Dk Magufuli akimfariji mtoto wa marehemu Dk Kigoda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro akimfariji dadake na marehemu Dk Kigoda, Dk Aisha Kigoda.
 Mkuu wa Mkowa wa Tanga, Mwantumu Mahiza akimfariji mjane wa marehemu Dk Kigoda, Rasul Kigoda
 Dk Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue wakati wa mapokezi ya mwili wa marehemu Dk Kigoda Uwanja wa Ndege.
 Dk Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kuupokea mwili wa marehemu Dk Kigoda
Dk Magufuli (kulia) akiangalia jeneza lenye mwili wa Dk Kigoda ukishushwa wakati wa mapokezi ya mwili huo kwenye Uwanja wa Ndege, Dar.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages