Msafara wa mgombea wa Urais
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe
Magufuli ukishuka kwenye kivuko cha Kamanga wilayani Sengerema mkoani
Mwanza wakati mgombea huyo alipowasili wilaya ya Sengerema kwa ajili ya
mikutano yake ya kampeni katika jimbo la Buchosa na Geita Vijijini
ambapo amewahutubia wananchi katika mikutano miwili mikubwa ambayo
imefanyika katika miji ya Nyehunge wilayani Sengerema na Nkome mkoani
Geita.
Watu wengi wenojitokeza kwenye
mkutano hiyo ambapo Dk. John Pombe Magufuli aliomba kura za ndiyo kwa
wananchi ili wamchague na kuwa rais wa Tanzania katika uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu
nchini kote ukishirikisha vyama vingi vya siasa
Dk John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi hao ambao wengi wao ni wavuvi amewaomba kutofanya
uvuvi haramu kwani unasababisha kuua samaki na mayai yake jambo ambalo
linapunguza samaki ziwani na kuwafanya wakose biashara lakini pia
watakosa kitoweo.
Ameongeza kwamba Sangara mmoja
anataga mayai zaidi ya milioni moja au milioni moja na laki tano, ukiua
sangara kumi kwa bomu ni sawa na kuua samaki milioni kumi au kumi na
tano ambao wangezaliwa jambo ambalo ni hasara kubwa kwa maliasili zetu
za Samaki.
“Ninawaomba kura Ndugu zangu
lakini lazima niwe mkweli na msema kweli ni mpezi wa Mungu, wavuvi
wachache wanaofanya uvuvi haramu watubu na kuacha kazi hiyo. Kwani
serikali yangu itaongozwa kwa kufuata sheria na Busara ya hali ya juu
ili kuwafanya watanzania hasa wa maisha ya kawaida waone faida ya
maliasili zao”.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE -NKOME-GEITA
Msafara wa mgombea wa Urais
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe
Magufuli ukiongoza na jeshi la polisi ili kuhakikisha usalama.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akielekea
nje ili kusalimiana na wananchi wa kivuko cha Kamanga waliojitokeza
waliojitokeza kumlaki.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wakazi wa Kamanga mara baada ya kuwasili akitokea jijini
Mwanza
mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi na kuomba kura katika mji wa Nyehunge jimbo la
Buchosa mkoani Mwanza.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Umati wa wananchi wa Nyehunge
Buchosa wakimshangilia mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika
mkutano wa kampeni.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea ubunge wa jimbo la Buchosa Mh. Charles Tizeba katika mkutano wa
kampeni uliofanyika mjini Nyehunge.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea ubunge wa jimbo la Buchosa Mh. Charles Tizeba wakati
alipomuombea kura katika mkutano wa kampeni uliofanyika Nyehunge.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa
amekaa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na mjumbe wa kamati ya
ushindi ya CCM Mh. Anthony Dialo kulia na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Geita na mgombea ubunge jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku
Msukuma katikati katika mkutano wa kampeni uliofanyika mji wa Nkome
Geita vijijini.
Baadhi ya wananchi wenye ulemavu
wakimshangilia Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akihutubia
mkutano wa kampeni mjini Nkome Geita vijijini.
Kundi la Makomando likitoa burudani katika mkutano huo.
Msanii Malaika akifanya vitu vyake katika mkutano huo.
Kundi la Orijino Kemedi likionyesha vitu vyao jukwaani.
Masanja Mkandamizaji na Mpoki wakihutubia wananchi kama kawaida yao.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano huo mjini Nkome.
Mbwembwe za kampeni kama unavyowaona katika picha.
Mgombea wa Urais Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa mbali
akionekana wakati alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi mjini Nkome
Geita Vijijini.
Picha mbalimbali zikionyesha maelfu ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269