Breaking News

Your Ad Spot

Oct 17, 2015

DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA MBUNGE WA JIMBO LA LUDEWA, MKOANI NJOMBE DEO FILIKUNJOMBE HAULE,

Rais Kikwete akizungumza  wananchi wa Bagamoyo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Rais Dk.Jakaya Kikwete akifungua pazia kwa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza wananchi wa Bagamoyo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza  wananchi wa Bagamoyo juu ya ujenzi wa bandari ya Bangamoyo. 
Makamu wa Rais Mtendaji wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China, Dk.Hu Jianhua akizungumza katika uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo . 
Sehemu ya viongozi wa waliohudhuria uwekaji wa jiwe la la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo .
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi mbalimbali baada ya kuweka jiwe la msingi na ujenzi wa bandari ya bagamoyo .
Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
RAIS  Kikwete ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kufanya tathimini upya kwa wakazi wa vijiji vitatu wanaopisha bandari ya Bagamoyo.
Dk.Kikwete ameyasema hayo  Bagamoyo wakati wa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ,amesema kuwa wananchi wasiondoke katika maeneo yao wakiwa na manunguniko.
Amesema kuwa mradi wa ujenzi ni mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kupewa haki yake kutokana na eneo ikiwa pamoja na kujengewa nyumba katika kuanza upya kwa makazi ya Kidagoni.
Rais Kikwete amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo umekuja wakati mwafaka kwa kuongeza fursa nyingi baada ya kukamilika kwa mradi huo na kuongeza uchumi wa nchi.
Aidha ameiagiza Mthamini wa Halmashauri kutafutiwa sehemu nyingine kutokana na kufanya tathimini isiyoendana na malipo hali ya wakazi hao ambao wameachia eneo hilo kwa ajili ya uchumi.
“Nchi haiwezi kuwa safi kuwepo mradi mkubwa wa bandari kubwa Afrika lakini wananchi waliocha eneo hilo wakiwa wananungunika kwa kupuchwa mali zao kwa ajili ya mtu mmoja tu”amesema Rais Jakaya. 
( Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages