.

MAGUFULI APANIA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA WAKAZI WA WILAYA YA KIBAHA ,DAR,MORO,KWA KUJENGA NJIA SITA

Oct 23, 2015

indexg 
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
………………………………………………..
MGOMBEA Urais  kupitia  tiketi ya Chama  cha mapinduzi (CCM) Dr. John  Magufuli amewahakikishia wananchi wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani endapo akipewa lidhaa ya kuongoza nchi ni lazima atimize azma yake ya kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kujenga njia sita za lami kuanzia Jijini Dar es Slaam kupitia maeneo ya  , mlandizi, chalinze mpaka mkoani  morogoro ili kuondokana na changamoto ya msongamano wa magari.
Magufuli aliyasema hayo wakati wa alipofanya mikutano yake miwili ya hadhara  katika jimbo la kibaha vijijini pamoja na jimbo la kibhaa mjini ambapo alidai kuwa ana imani miundombinu ya baarabara ikitengenezwa katika kiwango kinachotakiwa kinatweza kuleta fursa ya wafanyabishara kusafirisha mizigo yao na biashara kwa urahisi na kuweza kukuza uchumi.
 Aidha Magufuli alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha anapamabana kufa na kupona ili kuweza kuondoka na msongamano wa foleni ya magari  ambao umekuwa ni kero ya siku nyingi katika barabara ya morogoro hivyo kukamilika kwa ujenzi huo wa njia nsita  kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa waananchi wa kibaha pamoja na Taifa zima kwa ujumla.
“Mimia hapa napenda kuwahakikishia wananchi  wa kibaha kwa kushirikiana na Silvestry koka kuwa hii kero ya msongamano ya magari katika barabara hii tutaitafutia suluhisho la kudumu na pindi tukiazna kazi ni lazima tuweke mipango madhubuti ambayo itaweza kuleta mabadiliko na kupunguza adha ya kero ya foleni ambayo ilikuwa hapo awali.,”alisema Magufuli.
Dr Magufuli akifafanua zaidi juu ya suala hilo alisema kwamba katika kupamabana na changamoto hiyo ya msongamano wa foleni serikali ya wawamu ya nne tayari imeshaanza jitihada zake za hali na mali ambapo katika kukabilina suala hilo mizani ya maili moja mabyo ilikuwa ni inachangia kwa kisi kikubwa kuwepo kwa foleni imeamishia katika eneo la vigwaza.
“Hapa kwanza nilipo wananachi wa kibaha mmenifurahisha sana kwa kuonyesha upendo wa dhati kwa mapokezi makubwa ambayo kiukweli nimefarijika lakini kitu kikubwa mabcho nitakisimamia ni uboreshaji wa miundombinu ya barabara ili zimweze kupitika na hili nitalivalia njuga kweli kweli nikisaidiana na Koka ambaye amewza kufanya mabadiliko makubwa katika kipindi chake cha uongozi hivyo wananchi inapaswa kuhakikisha mnampa kura nyingi yeye, madiwani pamoja na mimi mwenyewe maana hapa ni kazi tu,”alisisitiza Magufuli.
Pia alisema kwamba endapo mji wa kibaha ukiwa barabara nzuri ambazo zinaweza kupitika kwa urahisi bila ya kuwa kero kutaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kupunguza na msongamano ambao umekuwa ukijitokeza katika jiji la Dar es Salaam, hivyo juhudi zake zote ni kuuendeleza mji wa Kibaha ambao utaweza kuleta chachu ya kimaendeleo .
Mgufuli  aliwaambia wananchi anao uzoefu mkubwa katika wizara mbali mbali kwani alishawahi kuwa waziri wa  ujenzi katika kipindi cha miaka 15 hivyo ana imani endapo akiwa rais atahakikisha katika siku zausoni ataweka  mipango kabambe  kwa kujenga barabara nyingine za juu zaidi zaidi ya  saba ambazo lengo lake kubwa ni kuondokana na usumbufu wa  msongamano ambao umekuwa ni kero ya siku nyingi sana.
Akizungumzia kuhusiana na suala la ardhi Mgufuli alisema kwamba serikali yake itahakikisha kwamba wananachi ambao wenye maeneo yao atawasimamia kwa hali na mali ili kuweza  kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo katika baadhi ya maeneo inatokana na kugombania maeneo kati ya wananchi na wawekezaji.
Awali Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha (CCM) Silvestry  Koka alimwakikishia Mgombea urais huyo kuwa atahakikisha changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kibaha mjini atazifanya kazi kwa hali na mali ikiwemo kuhakikisha wanapata huduma zote muhumi zinasotakiwa ikiwemo, maji, afya, elimu, miundombinu pamoja na kusimamia kikamilifu suala la wagonjwa wanaofanyiwa vitendo vya unayanyasaji.
Koka pia aliongeza kuwa katika kuhakikisha anapambana na janga la umasikini ataviwezesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali  kwa upande wa vijana na wakinamama kwa kuwapatia mitaji ambayo itaweza kuwasaidia kuachana na kuwa tegemezi , na kuongeza kuwasaidia wazee ambao wamekuwa wakibaguliwa katika kupatiwa huduma ya afya.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª