Breaking News

Your Ad Spot

Oct 28, 2015

MATUKIO MBALIMBALI YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015


11.00am:Mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA Edward Lowassa atarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari mda wowote kuanzia sasa
10.30am:Chama cha ACT Zanzibar
Chama cha Uzalendo cha ACT kisiwani Zanzibar kimeiandikia barua tume ya uchaguzi kisiwani humo ZEC kikiitaka kutoa matokjo ya uchaguzi kwa haraka.Chama hicho kupitia naibu wake Ali Makame kinasema kuwa kutotolewa kwa matokeo hayo kunaathiri huduma kwa wananchi.

10.00am:Vichwa vya habari vinavyogonga magazetini nchini Tanzania.
9.30am:Chama cha CCM kinachoongozwa na mgombea wa urais John Magufuli kimeshinda majimbo yote ya ubunge katika eneo la Dodoma huku muungano wa Ukawa chini ya uongozi wa Edward Lowassa ukichukua viti vingi katika mji wa Dar es Salaam.
9.00am:NEC yatoa ufafanuzi kuhusu matokeo

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya rais kutoka majimbo mbalimbali akisema kuwa tume hiyo inatoa matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo yote nchini..Ameongezea kwamba hakuna mgombea wala chama kinachopendelewa katika suala la kutangazwa kwa matokeo na kwamba mshindi atapatikana tu kupitia kura nyingi.
7.00am:Washerehekea Kinondoni
 Kulikuwa na sherehe katika jimbo la Kinondoni nchini Tanzania baada ya chama cha CUF kushinda katika eneo hilo.
Vijana waliokuwa wakifurahia ushindi huo waliimba na kuzunguka na bajaji wakiusifu ushindi huo na chama chao.
Hatahivyo maafisa wa polisi katika eneo hilo walifika katika eneo hilo na kuhakikisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea.
6.00am:Hali ya wasiwasi yatanda Zanzibar
Hatua hiyo inalenga kupunguza hofu na wasiwasi uliotanda hasa baada ya machafuko kushuhudiwa huko.
Vyombo vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na hali ya sintofahamu iliyosababishwa na mgombea wa urais wa upinzani kujitangaza kuwa mshindi.
Hatua hiyo ya imelaaniwa vikali na chama tawala cha CCM kilichotoa shinikizo kwa tume ya uchaguzi kuchukua hatua kali dhidi yake.
UMEAMKAJE?
Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Tanzania yanaendelea kutolewa huku BBC ikiendelea kukufahamisha kuhusu matukio tofauti nchini humo. Tume ya Taifa ya Uchaguzi jana ilitangaza matokeo ya majimbo takriban 100 na matokeo zaidi yanatarajiwa leo.
Tunafuatilia pia hali ilivyo Zanzibar baada ya mtafaruku jana kuhusu kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wakati mmoja maafisa wa usalama walizingira kituo kinachotumiwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutangaza matokeo na hakuna aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka. Tume ya uchaguzi humo visiwani kufikia jana jioni ilikuwa imetoa matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo yote 54.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages