.

MSANII WA COKE STUDIO APONGEZWA KWA KUSHINDA TUZO

Oct 23, 2015

Msanii aliyeshiriki katika msimu wa tatu wa Coke Studio unaoendelea kuoneshwa Clouds TV Vanessa Mdee, amepongezwa kwa kupata tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki kwenye tuzo za Afrimma zilizofanyika Marekani hivi karibuni.

Pongezi hizo zimetolewa na kampuni ya Coca-Cola ambayo inaendesha onyesho la kusisimua ya muziki la Coke Studio ambalo linaendelea nchini kupitia luninga ya Clouds na kuwavutia watazamaji wengi wa muziki nchini ikiwemo nchi nyingine za Africa.

Meneja wa Biashara za Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka amesema kuwa wanajivunia kuona mshiriki wa Coke Studio mwaka huu anazidi kupata mafanikio kwa kushinda tuzo nyingine zaidi.

“Mafanikio ya Vanessa yametufurahisha sana akiwa ni mmoja wa wasanii wa Coke Studio mwaka huu tuna imani naye kubwa kuwa ataendeleza kipaji chake cha muziki na kuweza kupata mafanikio zaidi.

Wasanii wanne kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu  ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na  mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, Fid Q amefanya bonge la kolabo (mash-up) na Maurice Kirya kutokana Uganda, Gwiji wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amefanya kolabo matata(mash-up) na Victoria Kimani kutoka nchini Kenya na wakati Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na  mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face.

Wanamuziki wengine wa Tanzania  walioshinda tuzo za Afrimma ni Diamond Platnumz ambaye alifanikiwa kukomba tuzo 3 ambazo ni Video bora ya kucheza NANA, Msanii bora wa Afrika Mashariki na msanii wa mwaka, Diamond pia alishiriki kwenye msimu wa pili wa Coke Studio mwaka jana.

Ommy Dimpoz naye alijishindia tuzo ya msanii bora anayechipukia.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช