Breaking News

Your Ad Spot

Oct 23, 2015

NEWALA WAHAKIKISHIWA USALAMA WA KUTOSHA KWA RAIA NA MALI ZAO SIKU YA UCHAGUZI

 Na Father Kidevu Blog
……………………………….. WANANCHI wilayayani
Newala wamehakikishiwa usalama wa kutosha siku ya kupiga kura na kutakiwa
kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wao bila wasiwasi wowote.
Akizungumza na
Habarileo kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala
amesema wakazi wa Newala husususani katika majimbo ya uchaguzi ya Newala Mjini
na Newala vijini wasiwe na hofu juu ya amani siku ya kupiga kura.
“Nitumie nafasi hii
kuwatoa hofu wananchi na kuwahakikishia usalama wenu na mali zenu, kwamba siku
ya kupiga kura hakutakuwa na vurugu zozote, Hivyo wale wote waliojiandikisha
kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura siku hiyo bila wasiwasi
wowote,”alisema Magala.
Magala amesema wananchi
waendelea kuilinda na kuitunza amani katika kipindi hiki cha kumalizia kampeni
na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi pasipo kuvuruga
amani na utulivu uliopo Wilayani humo.
“Katika kipindi hiki
cha kumalizia kampeni na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi,
tuendelee kuitunza amani iliyopo katika Wilaya yetu; upendo na mshikikamano
tuliona siku zote tuuimarishe zaidi kipindi hiki ili tuvuke salama na kubaki
salama baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika,”alisema Magala.
Aidha amesema Serikali
imejipanga vizuri kuimarisha doria katika kipindi cha  siku za mwisho za kampeni, wakati wa uchaguzi
na baada ya uchaguzi.
Magala amesema ni haki
ya kila mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura kutimiza haki yake ya kumchagua
kiongozi anayemtaka katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika mazingira
tulivu yasiyo nafujo na hivyo kuwataka wananchi kufanya hivyo na wakishapiga
kura warudi majumbani na kusubiri kutangazwa matokeo.
“Niwatahadharishe, kama
wapo, Wananchi wanaokusudia kuvuruga Uchaguzi kwa namna yoyote ile kwamba
Serikali haitawavumilia. Hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao. Vyombo vya Ulinzi vyote vipo ‘standby’
kuhakikisha utulivu unakuwepo wakati wa kwenda kupiga kura na baada ya Uchaguzi
kukamilika,”alisema Magala.
Magala pia amewaomba wananchi
kutoa taarifa kwa viongozi watakaokuwa jirani nao au vyombo vyausalama
vitakavyokuwa karibu, pale watakapoona dalili zinazoashiria kuvunjika kwa amani
na kuwataka wachague viongozi bora, waadilifu, wachapaka kazi, watakao waletea
maendeleo katika maeneo yenu ya Kata na Wilaya yetu ya Newala kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages