Matokeo ya ukaguzi wa kimatibabu
uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina Faso marehemu
Thomas Sankara miaka 28 baada ya kuuawa,yanaonyesha kuwa mwili wake
ulijaa risasi kulingana na wakili aliyekuwa akiwakilisha familia yake
kulingana na mtandao wa facebook wa kituo cha habari cha Burkina 24.
Familia
yake ilikuwa ikingojea matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo
yalikuwa ya bwana Sankara,wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya
habari nchini humo
Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa
miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987,na alizikwa kwaa
haraka kufuatia mpinduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore.


No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269