Breaking News

Your Ad Spot

Oct 28, 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI




JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 158 KWA MAKOSA YA KUFANYA FUJO, VURUGU NA KUHARIBU MALI WILAYA YA RUNGWE.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 38 KWA KUFANYA VURUGU NA UHARIBIFU WA MALI WILAYA YA MBOZI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA: MNAMO TAREHE 25.10.2015 KUANZIA MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HADI SAA 16:00 JIONI KULIFANYIKA UCHAGUZI MKUU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WABUNGE NA MADIWANI. KATIKA JIMBO LA RUNGWE, NDUGU SAUL H. AMON KWA TIKETI YA CCM NA NDUGU JOHN MWAMBIGIJA KWA TIKETI YA CHADEMA NDIO WALIOKUWA WAKICHUANA VIKALI KUGOMBEA KITI HICHO. WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA KUFANYIKA KATIKA OFISI YA UCHAGUZI JIMBO LA RUNGWE WATU WENGI NA KATIKA HAO WALIKUWEPO WAFUASI WA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA NDUGU JOHN MWAMBIGIJA WALIKUSANYIKA NJE YA JENGO LA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE HUKU NA HAO WAFUASI WA MWAMBIGIJA WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA DHIDI YA MGOMBEA WA CCM, MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA JESHI LA POLISI AMBAO WALIKUWEPO PALE KUHAKIKISHA KUNAKUWEPO HALI YA AMANI NA UTULIVU WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIENDELEA. ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI WAFUASI HAO WALIKUWA WAKIIMBA NYIMBO ZA KASHFA AMBAO ILIONEKANA WAMETOKA WALIOKUWA SEHEMU MBALIMBALI KAMA VILE RUNGWE, MBEYA MJINI, TUNDUMA NA MAKETE WALIANZA KUFANYA FUJO NA VURUGU KWA KUWAZOMEA ASKARI NA KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA MAWE, CHUPA NA FIMBO KWA MADAI YA KUTAKA MATOKEO YATANGAZWE WAKATI ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIWA LINAENDELEA.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages