Breaking News

Your Ad Spot

Oct 30, 2015

UKAWA WATAKIWA KUKUBALI MATOKEO YA URAIS

 Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa Mkutano wa Plicy Forum walipokuwa wakiongelea Ilani yao na Asasi za kiraia kutoa malengo yao makubwa  kwa Rais wa awamu ya tano mambo muhimu ayape kipaumbele ikiwemo Katiba, Usimamizi wa Rasilimali za Nchi na NK. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Mkurugenzi wa Ahadiway Life Development Initiateve (NGO) Team James Obedi (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano huo kumalizika Dar es Salaam na wakwanza kulia ni Mwanafunzi wa Sheria katika Chuo cha Royal kilichopo Dar es Salaam, naye aliitaka Serikali ya awamu ya tano itengeneze miundombinu ya kuwanufaisha Wananchi kuongeza uzalendo baina ya wananchi na Viongozi  kuwepo kwa Katiba  Mpya ambayo itakuwa inatowa muongozo na Dira ya Taifa. Serikali itunge Sera ya Taifa, kuliko kila Chama kuja na Sera yake, kuwepo na mwendelezo wa upanuzi wa viwanda, vitakavyo saidia kukuza uchumi wa Nchi kwa kizazi kilichopo na kijacho 


 Wadau
 Afisa Programu Idara ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera. (HAKI ELIMU) Makumba Mwemezi (wa pili kulia) wakishauriana jambo na wadau wakati wa mkutano huo


  Afisa Programu Idara ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera. (HAKI ELIMU) Makumba Mwemezi (wa pili kulia) akitowa mada katika Mkutano huo













Ukawa watakiwa kukubali matokeo ya urais

                                        Salha Mohamed

MRATIBU wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa ameutaka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kukubaliana na matokeo ya nafasi ya mgombea urais aliyotangazwa juzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Pia aliutaka umoja huo kuandaa mkutano wa kitaifa ili kuonesha shukrani zao kwa wananchi waliowapigia kura kwani wamepata kura nyingi tofauti na waliovyofikiria kwa jamii hizo kutaka mabadiliko.

Akizungumza Dar es Salaam , Mratibu huyo alisema umoja huo unapaswa kukubali ushindi wa Dk. John Magufuli ingawa kulalamika ni haki yao huku akibainisha mfumo uliopo hauruhusu kupinga na kuonesha hisia zao.

"Hakuna njia nyingine ya kulalamika lakini pia wamekuwa waungwana kwa kutoandamana barabarani ambapo waliwataka vijana kutulia na si kufanya fujo mitaani ili kuhatarisha amani nchini,"alisema.


Alisema kutokana na matokeo hayo hategemei kuona mambo ya visasi ambapo kama mtu anaona ameonewa afuate taratibu za kisheria kama ilivyo katika nafasi ya ubunge na udiwani ingawa mfumo hauruhusu kupinga matokeo ya urais.

"Tumeshakuwa taifa moja kuna maisha baada ya uchaguzi siasa zimekwisha waliopata wafanye kazi, lililopo waliokosa wajipange mwaka 2020,"alisema na kuongeza kuwa umoja huo umepata ushindi mkubwa kama ambavyo hawakutegemea na kutokana na mifumo iliyopo.

Alisema wananchi wameukubali umoja huo kwa kuonesha kuwapigia kura nyingi na kupata wabunge na madiwani wengi tofauti na hapo awali  hasa ujio wa Lowasa kwani tofauti na hapo hali ingekuwa mbaya zaidi walipokuwa haw kwa vyama hivyo.

Aidha alisema wananchi wasiwe na hasira kwa kutopiga kura baada ya miaka mitano kwani walitaka mabadiliko hali iliyowafanya kuisumbua CCM.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages