Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2015

ORODHA YA WACHEZAJI 10 WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA (WANAOCHEZA AFRIKA)

Mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo hiyo anayecheza katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samata
Mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo hiyo anayecheza katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samata.
Siku moja baada ya Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) kutangaza majina ya wachezaji kumi watakaowania tuzo ya mchezaji bora barani Afrika, hatimaye wametangaza majina ya wachezaji kumi (10) watakaowania tuzo ya mchezaji bora anayecheza Afrika.
Katika orodha hiyo kwa mara ya kwanza Tanzania tumefanikiwa kuingiza mchezaji mmoja, Mbwana Ally Samata anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe inayoshiriki ligi kuu ya nchini Congo DRC.
Orodha ya wachezaji hao ni kama ifuatavyo;
  1. Abdeladim Khadrouf (Morocco-Moghreb Tetouan))
  2. Felipe Ovono (Equatorial Guinea- Orlando Pirates)
  3. Kermit Erasmus (South Africa- Orlando Pirates)
  4. Mbwana Ally Samatta (Tanzania – TP Mazembe)
  5. Mohamed Meftah (Algeria – USM Alger)
  6. Modather Al Tayeb (Sudan – Al Hilal)
  7. Robert Kidiaba (Congo DRC – TP Mazembe)
  8. Robert Assele (Ivory coast – Sewe Sports)
  9. Zinnedine Ferhat (Algeria – USM Alger)
  10. Baghdad Bounedjah (Algeria – Etoile Sportive Sahel)
Mchezaji bora katika orodha hiyo atapatikana kwa upigaji wa kura zitakazopigwa na makocha wa timu za taifa pamoja na wakurugenzi wa ufundi na tuzo hizo zinataraijwa kutolewa Januari, 7 2016 katika jiji la Abuja nchini Nigeria.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages