Breaking News

Your Ad Spot

Dec 2, 2015

MAAFISA WATENDAJI WAKUU WA MASHIRIKA YA NDEGE WAIPONGEZA TAA KWA JENGO JIPYA LA JNIA TBIII

 Sehemu ya jengo jipya la TBIII (au terminal III) la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, likionekana huku ndege moja ya kimataifa ikipita jirani yake Novemba, 2015. Wadau wa sekta ya usafiri wa ndege, ambao ni Maafisa Watendaji na Mameneja wawakilishi wa mashirika hayo walioko hapa nchini, walipata fursa ya kutembelea jengo hilo Jumatatu Novemba 30, 2015 ili kujionea wenyewe na kupata taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, litakalokamilika mwakani 2016. Jengo hilo litakalokuwa na teknolojia ya kisasa katika kuendesha mambo yake na kuhuduamia abiria, litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka mara tatu zaidi ya jengo la sasa yaani Terminal II linalohudumia abiria milioni 2.5 tu kwa mwaka. Kutokana na ongezeko hilo kubwa la abiria, wadau hao
wameiomba serikali kupanua Barabara ya Nerere inayoelekea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kufuatia kukaribia kukamilika kwa ujenzi wa jengo jipya la abiria (Terminal III au TBIII), la uwanja huo.
Ombi hilo walilitoa baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Akielezea zaidi maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa mradi huo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, Mhandisi Mohammed Milanga alisema, jingo la sasa la JNIA, terminal II, lina uwezo wa kuhuduamia abiria milioni 2.5 tu na kwamba katika jengo jipya, huduma mbalimbali zitapatikana kwa utaratibu utakaowawezesha abiria kufurahia uwepo wao kwenye uwanja huo.
Baada ya kutolewa takwimu hizo, Maafisa hao watendaji walionyesha wasiwasi wao ni kwa vipi barabara ya sasa ya Nyerere ambayo huelemewa kwa foleni na itaweza vipi kuwasaidia abiria kufika kwa wakati kutokana na ongezeko hilo la abiria.




MKUU wa Idara ya Masoko wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA,Bi. Scolastica Mukajanga, (wapili kushoto), akiwaeleza jambo wadau wa sekta ya usafiri wa anga, ambao ni Maafisa watendaji wakuu, CEOs wa Mashirika ya ndege wakati walipotembelea uwanja mpya wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal III jijini Dar es Salaam, Novemba 30, 2015.Wadau hao wameipongeza TAA kwa mapinduzi ya miundombinu kwa kupanua uwanja huo mkubwa kabisa hapa nchini na kuelezea kufurahishwa kwao kutokana na mipango iliyoelezwa na wasimamizi wa ujenzi wa jingo hilo kuwa utazingatia wadau wote kuwa na ofisi na sehemu mbaklimbali za kijamii. (Picha na K-VIS Media/Khalfan Said)

 Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akiwaeleza hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo, wadau hao
 Msaidizi wa Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la JNIA-TBIII, Mhandisi Caroline Ntambo, (wapili kulia) kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, akimsikiliza mmoja wa maafisa wakuu wa shirika la ndege la Qatar Airways, wakati maafisa hao walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo la TBIII
 Maafisa na wahandisi wa TAA
 Wakiangalia michoro na taarifa mbalimbali za ujenzi wa jengo
 Ziara ya jengo
 Picha ya pamoja


 Wadau na maafsia wa TAA, wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa jengo hilo iliyokuwa ikitolewa na Mhandisi Mohammed Millanga
Wakati wa maswali na ufafanuzi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages