Breaking News

Your Ad Spot

Dec 27, 2015

MZEE NJEMBA ANATAFUTWA, AMETOWEKA NYUMBANI KWAKE MAGOMENI

Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani) ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es salam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015.
Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.
Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf anayepatikana katika namba 0784 606 262.
Wanatanguliza Shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages