Breaking News

Your Ad Spot

Jan 14, 2016

AIRTEL YAZINDUA DUKA LA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua duka la kisasa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa kutanua wigo wa kutoa huduma zenye ubora tofauti na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake
Duka hilo la kisasa liko katika ofisi za makao makuu ya Airtel barabara ya Moroco.
   Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Sunil Colaso alisema” Tunayodhamira ya kuwa karibu na wateja wetu ili kuwapatia huduma bora zinazokidhi mahitaji yao.
    Duka letu jipya tulilolizindua leo litakuwa na sehemu maalumu itakayowawezesha wateja wetu kuona bidhaa bora za mawasiliano zikiwemo simu za aina tofuati na kupata nafasi ya kuzijaribu kwanza ili kuona ubora wake na kufanya chaguo la ununuzi. tunaamini wateja wetu sasa wateweza kufurahia huduma zetu kwa kuwa watapata nafasi ya kuchagua aina ya kifaa au simu wanayomudu kuitumia kwa urahisi zaidi”.
    “Duka letu la Airtel Expo litakuwa ni sehemu ya maonyesho na ubunifu kwa wateja wale wanaopenda kuishi maisha yanayoendana na technolojia ya kisasa ndani ya sekta ya mawasiliano. Kila atakaetembelea duka hili atafurahia huduma za haraka toka kwa watoa huduma wetu ambao watatatua mahitaji na matatizo yao katika mazingira ya kirafiki zaidi” alieleza Colaso.
      Akizindua duka hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani alisema “Ninawapongeza sana Airtel kwa kutengeneza duka hili la kisasa na kibunifu litalorahisisha utoaji huduma kwa wateja na watumiaji wa huduma za mawasiliano na kuchochea matumizi ya  technologia ya mawasiliano katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi ”
  “Natoa wito kwa wakazi wa Dar es saalam na wateja wa Airtel kutembelea duka hili na kufurahia mazingira bora na kuunganishwa na huduma za kifedha na huduma zote za mawasiliano nilizoziona hapa. alimaliza kwa kusema Mh, Ngonyani.
   Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja , Adriana Lyamba alisema “Duka letu litakuwa linatoa huduma kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa muda saa 3 hadi saa 11 jioni na Jumamosi kuanzia saa 3 hadi saa 7 mchana.            Huduma zote muhimu kama Airtel Money, huduma ya intanet, bidhaa za kisasa kwa Intaneti na  vifaa vya Wi-Fi yaani (Home Wi-Fi)  pamoja simu za smartphone za vitapatikana katika duka letu.”
     Adriana aliongeza kwa kusema Duka letu la Airtel Expo lina sehemu maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wateja watu maalum yaani (Airtel Premeir Custumers) ambapo mteja anaweza kupitia na kusaini mikataba wake au kulipia ankra yake, kurudisha namba iliyopotea, huduma za Airtel Money na nyingine nyingi zitatolewa.”
     Kuzindulia kwa duka hili ni muendelezo wa kutimiza dhamira na mkakati wa Airtel wa sasa wa kukamilisha maduka 28 yanayoendelea kutengenezwa na kuzinduliwa nchi nzima hadi ifikapo  Juni mwaka huu.
 Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,( kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw. Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya
 Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa  na simu mbalimbali vinavyopatikana  katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel  Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa  na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Eng, Edwin Ngonyani akimsikiliza Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel, Bi Adriana Lyamba na meneja huduma kwa wateja Zakia Omary (katikati) wakati wa uzinduzi  rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel  Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages