Breaking News

Your Ad Spot

Jan 9, 2016

ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA KATOLIKI LA DAR ES SALAAM, MWADHAMA POLYCARP KARDINALI PENGO ASIFU HUDUMA ZA TAASISI YA MOYOYA JAKAYA KIKWETE

1
 Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili, ambapo amepongeza weledi wa huduma  za madaktari na wauguzi kutokana na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
2
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
3
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
4
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili kutoka kushoto ni Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo na Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,  Dkt. Mpoki Ulisubisya na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Ummy Mwalimu
5
Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  akimshukuru  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  kwa kutoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari  na wauguzi wa Taasisi hiyo ya moyo kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Ummy Mwalimu
6
Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete akiwafafanulia waandishi wa habari mambo mbalimbali waliyotaka kujua kuhusu taasisi hiyo katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Ummy Mwalimu na  kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dkt. Mpoki Ulisubisya.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages