Breaking News

Your Ad Spot

Jan 25, 2016

KLOPP AVUNJA MIWANI AKISHANGILIA USHINDI WA LIVERPOOL

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool jana alijikuta akiharibu miwani yake mara baada ya kujumuika pamoja na wachezaji wake kushangilia goli la ushindi katika dakika za mwisho za mchezo wao dhidi ya Norwich uliomalizika kwa ushindi wa magoli 5-4.
Adam Lalana alifanikiwa kuwa shujaa wa mchezo mara baada ya kufunga kwa shuti kali dakika ya 95 ya mchezo dakika chache kabla ya Sebastian Bassong kuisawazishia Norwich na matokeo kuwa goli 4-4.
Kocha Jurgen Klopp anasema ni mara ya pili sasa anaharibu miwani yake kwani anakumbuka Nuri Sahin wakiwa Borussia Dortmund alimrukia wakishangilia ushindi dhidi ya Bayern Munich, na jana ikawa ni Adam Lalana.
Lakini pamoja na ushindi huo, kocha huyo mjerumani Jurgen Klopp 48, hakufurahishwa na performance ya timu yake kutokana na kuruhusu mabao mengi mepesi katika michezo yake minne mfululizo wakiruhusu bao 10 langoni mwao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages