Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al Maadadi
ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akisalimiana na na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al
Maadadi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam
Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al Najem, ofisini
kwake jijini Dar es salaam , Januari 13, 2016. (Pichana Ofisi ya Waziri
Mkuu)
…………………………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait.
Akizungumza kwa nyakati tofauti
na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia,
pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo
ameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar,
Abdallah Jassim al Maadad amesema Serikali yake itaendelea kuisaidia
Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza
kutoa msaada kwa Tanzania.
Amesema Quwait iko tayari
kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni
yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta
nyingine ambazo wangependa kuwekeza ni pamoja na sekta ya uvuvi na
viwanda.
Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al
Najem ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake
kupitia ‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Balozi Najem, pia ameshauri
vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano
zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269