Breaking News

Your Ad Spot

Jan 10, 2016

MBUNGE WA KIKWAJUNI, MASAUNI, ATEMBELEA MRADI WA MAJI KABURIKIKOMBE, ZANZIBAR

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Yussuf Masauni na Aliyekuwa Mwakilishi wa Rahaleo kwa sasa ni Mgombea Uwakilishi Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salim Jazira wakiteta jambo wakati wa ziara ya Mbunge Mhe Masauni kutembelea Mradi wa Maji kaburikikombe Zanzibar. 
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akiwa katika ziara yake kutembelea mradi wa kisima cha maji kaburukikombe migimbani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Tanzania Youth Icon Abdalla Ahmeid akizungumza kuhusiara na mradi mkubwa wa Kisima cha Maji kilichofadhiliwa na TAYI kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar wakati wa ziara ya Mhe Mbunge Hamad Masauni katika jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Wananchi wa Jimbo hilo wakati wa ziara yake katika mradi wa maji kaburi kikombe migombani Zanzibar Mradi huo unasimamiwa na Jumuiya ya TAYI  Tanzania Youth Icon kulia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo na kwa sasa anagombea Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Nassor Salim Jazira.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages