Breaking News

Your Ad Spot

Jan 12, 2016

NAIBU WAZIRI WA HABARI ANASTAZIA WAMBURA AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI

mek1
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati wa ziara ya Naibu Waziri aliyoifanya katika Wilaya ya Temeke kukagua viwanja vya wazi vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo ambavyo vimemiwa na baadhi ya wananchi. (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).
mek2
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Anastazia Wambura (kulia) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Said Meck Sadiki wakati wa ziara ya Naibu Waziri aliyoifanya katika Wilaya ya Temeke kukagua viwanja vya wazi vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo ambavyo vimevamiwa na baadhi ya wananchi. 
mek3
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Anastazia Wambura (kulia) akiagana na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Said Meck Sadiki tayari kuanza ziara ya kukagua viwanja vya wazi vilivyokusudiwa kwa ajili ya michezo vilivyovamiwa na baadhi ya wananchi.
mek4
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Waziri Kombo akimkabidhi Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Anastazia Wambura  taarifa ya utekelezaji kuhusiana na shughuli za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo za Halmashauri hiyo, kulia ni Mbunge wa jimbo la Temeke. Abdalah Mtolea na kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo,Salum Fesal.
mek5
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Anastazia Wambura wa pili kutoka kulia akikagua Uwanja wa Tandika ambao una mgogoro na wapangaji wa maduka ambapo aliagiza siku saba kwa wavamizi wote nchini kutoka kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kupisha shughuli za michezo, wa pili kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo . Salum Fesal.
mek6
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikono Arts aliyesimama, Henry Clemensi  akiongea na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura kuhusu shughuli wanazofanya ili kuwasaidia wasanii wa sanaa za uchongaji ikiwa ni pamoja na kuwatafutia soko nje ya nchi, wa kwanza kulia waliokaa ni Mbunge wa jimbo la Temeke Abdalah Mtolea na wa kwanza kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Salum Fesal.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages