5- Hili ndio kubwa lililonishangaza mtu wangu, baada ya kufika hoteli inayoitwa Amani Kendwa ambayo ipo pembezoni mwa fukwe za bahari ya hindi hapa Zanzibar nje kidogo ya mji wa Unguja.
Hii ni hoteli ambayo maalum kwa waitaliano tu kwa mtu mwingine
huruhusiwi kulala ila unaweza ukaenda kupata lunch au dinner hiyo haina
neno. Utaratibu wa muitaliano kupata nafasi ya kulala hapo ni ana book
moja kwa moja akiwa Italia na kupelekwa hapo, hivyo
watu wa mataifa mengine hawapokelewi kwa kulala zaidi ya kupata chakula.
Hata kama ni muitaliano ila umekuja kuomba ukiwa Zanzibar huwezi ruhusiwa kulala.

Mtu wangu wa nguvu wakati Kombe la
Mapinduzi likiwa limesimama kwa mapumziko ya siku moja kabla ya Jumapili
ya January 10 kuendelea katika hatua ya nusu fainali. Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kutembelea maeneo tofauti tofauti hapa visiwani Zanzibar, lengo likiwa ni kukujuza baadhi ya vitu ambavyo huenda ukawa huvijui kuhusu Zanzibar. Haya ni mambo matano ambayo yanaweza yakakushangaza kama umefika Zanzibar kwa mara ya kwanza na umezoea kuishi maeneo kadhaa ya mikoa ya Tanzania bara basi huenda hii ikakushangaza.
1- Kama umezoea kwenda maeneo ya Kariakoo kununua bidhaa na kuwekewa katika mifuko ya plastic, basi hilo Zanzibar
hakuna mifuko laini ya plastic inayoruhusiwa. Ukinunua bidhaa kuna aina
ya mifuko ambayo utapewa kama mifuko ile ya karatasi ya kaki, lakini
usitegemee kuona mifuko laini ya plastic ikizagaa au kutumika.

2- Daladala au mabasi ya abiria kwa Zanzibar
hayaruhusiwi kusimamisha abiria, hivyo mara nyingi husimamisha abiria
pale mahali ambapo hakuna askari. Ikitokea wamesimamisha abiria halafu
wanakaribia eneo kuna trafiki basi konda atakuomba ukae vizuri tu ili
gari isionekane kama imejaa kukwepa kusimamishwa na askari.

3- Vesper ndio pikipiki zinazotumika kwa wingi Zanzibar ila sio kubeba abiria ni kwa safari binafsi, usishangae kuona siku ikipita bila kuona aina nyingine ya pikipiki kama Boxer, Sanlg na nyinginezo na ukiziona basi ni kwa safari binafsi na sio kama Boda Boda.
![]() |
| 4- Kama ulikuwa unajua Hiace na Coaster ndio gari pekee zinazoweza kutumika kubeba abiria kama daladala basi utakuwa umekosea, Zanzibar hata Canter zimeruhusiwa kubeba abiria ila kwa mfumo ambao wamezitengeneza na kuziwekea mabenchi ndani na kazi ya kubeba abiria inaendelea kama kawaida. |


Sehemu ya muonekano wa fukwe za Amani Kendwa nyakati za usiku

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269