Breaking News

Your Ad Spot

Jan 22, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA TAMISEMI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene ikiwa ni ishara ya Ofisi hiyo kutambua mchango wake wa kuendeleza michezo wakati akiwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo . Mheshimiwa Majaliwa alizungumza na watumishi wa TAMISEMI mjini Dodoma Januari 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake Mjini Dodoma



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Georoge Simbachawene akizungungumza kabla ya kukaribisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzungumza na Wafanyakazi wa Tamisemi mjini Dodoma 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mjini Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wa Tamisemi baada ya kuzungumza  nao mjini Dodoma Januari 21, 2016.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Benard  Makali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi, Benard Makali baada ya kuzungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo mjini Dodoma Januari 21, 2016. Kushoto ni Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi , George Simbachawene na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, Eliudi Sanga. 
Waziri Mkuu akiagana na Waziri Simbachawene

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages